‘Gaza inashuhudia maafa ya kibinadamu ambayo hayajawahi kutokea’: Wizara ya Mambo ya Ndani





Ofisi ya vyombo vya habari vya serikali ya Ukanda wa Gaza ilisema kwamba hasara iliyopatikana kutokana na uvamizi unaoendelea wa Israel imepita jumla ya machafuko yote yaliyopita Gaza.

Siku ya Jumanne, ofisi ilieleza zaidi kwamba hasara hizi ni pamoja na hesabu ya vifo, majeruhi, na uharibifu wa nyumba na miundombinu.

Wamesisitiza kuwa, hali mbaya ya kibinadamu huko Gaza haina mfano wowote ikilinganishwa na vita vya zamani, na kuitaka jumuiya ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na za maana kukomesha mauaji ya kikabila yanayotekelezwa.

Msemaji wa shirika la Umoja wa Mataifa la Misaada na Kazi (UNRWA), alipokuwa akizungumza na BBC, alisema kuwa “vifaa vinapungua” huko Gaza, huku kukiwa na hofu “magonjwa yanayosababishwa na maji yataanza kuenea.”

Akizungumzia kile wanachoweza kutoa huko kusini mwa Gaza, mkurugenzi wa mawasiliano wa UNRWA Juliette Touma alisema, “Wanaendelea kutoa usaidizi popote inapowezekana. UNWRA imezidiwa. Tumezidiwa. Vifaa vyetu vinapungua na kuisha haraka.”

“Wafanyikazi wetu pia wamechoka sana. Wameathiriwa wenyewe na vita. Wengi wao wamepoteza wapendwa wao, kwa huzuni UNRWA tumepoteza wafanyikazi 14 na idadi hii inaendelea kuongezeka,” aliongeza.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad