Haji Manara Aiomba Serikali iingilie Kati Wizi Jezi za Simba na Yanga

 

Haji Manara Aiomba Serikali iingilie Kati Wizi Jezi za Simba na Yanga

Balozi wa Makampuni ya GSM, Haji Manara ameiomba Serikali kuingilia kati kuhusu masuala ya Jezi bandia zilizokamatwa jana Temeke Jijini Dar es Salaam.


Jezi za Klabu ya Simba na Yanga zimeshikwa na Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Yanga SC, Ally Kamwe .


Akizungumza na Manara TV, Manara amesema kuna haja ya Serikali kuingilia kati suala hilo la jezi maana timu peke yao haiwezi.


Manara amesema Mwanasheria wao Simon Patrick pamoja na Staff wengine wa Yanga SC wamelipambania suala hilo, lakini Serikali wanaweza kuwasaidia kuirahisi zaidi.


“Katika sura ya upole na unyenyekevu naiomba Serikali yetu itusaidie katika hili ambalo linahitaji nguvu yao katika kulitatua.


“Nalifahamu vyema suala hili, lakini sitaki kurudi nyuma wala kuanzisha upya. Tunaiomba serikali yetu kutusaidia katika hili,” alisema Manara.


Manara amefafanua kuwa wanaojihusisha na masuala ya kudurufu jezi wana mtandao mpana unaohusisha vitu vingi na taasisi mbalimbali kubwa.


“Rai yangu ni moja na hizi timu zinatumia kiasi kikubwa cha pesa katika kujiendesha na watu wengi wanasema mpira wetu umekuwa. Ishu sio kukua kwa mpira wetu, lakini vilabu hivi kuna watu wameweka pesa zao. Ghalib Said Mohamed (GSM) kwa Yanga SC na Mohamed Dewji (MO) wa Simba SC wameweka pesa zao nyingi.


“Hawa wote wameweka fedha. Yanga SC na Simba SC zamani zilikuwa mpata mpatae, angalau mauzo ya jezi hii imekuja kupunguza makali.


“Jezi zina thamani ya Sh. Bil 10. Naomba nirudie Serikali itusaidie. Vyombo vyetu viusaidie mpira. Maana nasikia kuna mtu mkubwa hagusiki, kiukweli hatuwatendei haki hawa kina MO na GSM.


“Kuitoa timu Tanzania kuipeleka nje ni kiasi kikubwa cha pesa cha pesa kinachotumika, alafu baadae tunakuja kusema vilabu vya Tanzania haviendelei, sio rahisi kuwa kiongozi mkubwa wa hizi timu, Sio rahisi wengi wanazungumza vitu ambavyo havipo.


“Sasa jezi zinaenda sokoni, lakini anatokea mtu na kuleta jezi bandia za Bil 10. Katika hili tunahitaji nguvu ya Kiserikali. Tukiliacha hili na likaishia hewani tutakuwa tumekwisha,” alisema Manara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad