Haji Manara Aipa Tano Simba "Wametupa Heshima"

 

Haji Manara Aipa Tano Simba "Wametupa Heshima"

Haji Manara aliyewahi kuwa Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Simba SC, amesema kitendo cha klabu hiyo kutolewa kwa Kanuni ya mabao ya kufunga na kufungwa dhidi ya Al Ahly imeiheshimisha Tanzania.

Simba SC wametolewa katika Mashindano ya African Football League na timu hiyo ya Misri kwa sare ya mabao 3-3, huku Al Ahly wakiwa na faida ya kupata sare ya 2-2 walipokuwa Jijini Dar es Salaam na 1-1 walipokuwa Jijini Cairo

“Kuna sura mbili hapa. Sura moja nimefurahi Simba SC kutuheshimisha, sura ya pili kama wangewatoa wale, sijui tungeweka wapi sura zetu” alisema Manara.

Manara amesema ingekuwa zamani kila mmoja angeona timu ya Tanzania inaenda kufungwa mabao matano dhidi ya Al Ahly, lakini sasa mambo ni tofauti.

“Zamani haikuwepo hiyvyo. Soka lao limesimama na sisi tumesogea, inakoendea tunaweza kuwatoa, Zamani ukisikia timu imeenda nje mnajua kuna mambo ya kufungana mabao matano “ alisema Manara.

Kwa upande mwengine @hajismanara amesema Yanga SC wanaweza kuibuka na ushinda katika pambano la Watani wa Jadi dhidi ya Simba SC, Novemba 05 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Manara amezichambua timu hizo na kusema Yanga SC hawampi mpinzani nafasi ya kulisogelea lango lao kiurahisi, tofauti na Simba SC wanaocheza kiulegevu.

“Hii ni mechi ambayo haitazami una ubora gani muda huo wa mechi yenyewe. Haitazami umetoka kucheza na nani na umemfunga nani.

“Tazama msimu Yanga SC walikuwa vyema, lakini alivyocheza na Simba SC alikuwa down na akapoteza mechi. Hii mechi ya keshokutwa Haiwezi kuwa mechi rahisi na kila timu iatataka kuonesha kitu, lakini nina uhakika Simba SC watafungwa “ alisema Manara.

“Wana kaulegevu fulani wanacho, Yanga SC hawana makosa. Nasema kama Al Ahly wangetumia nafasi walizozipata mechi yao ya Simba SC, mechi ingeweza kuisha hapa hapa Dar es Salaam.

“Lakini ukiwatazama Yanga SC wakishambuliwa hawaachi gape. Licha ya hivyo, hii inabakia kuwa mechi isiyotabirika maana unaweza kuwa na maandalizi bora, lakini ikatokea Majini mkashinda mechi,” alisema

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad