HATIMAYE Simba Wafunguka Ishu ya Kumtimua Robertinho

HATIMAYE Simba Wafunguka Ishu ya Kumtimua Robertinho

 

Kufuatia kelele kuwa nyingi kutoka kwa mashabiki zikiutaka uongozi umtimue kocha, uongozi wa Simba SC umefungukia ishu hiyo.


Ahmed Ally ambaye ndiye meneja wa habari na mawasiliano wa Simba SC, amesema Robertinho yupo sana na hawana mpango wa kumuacha leo wala kesho.


"Kocha wa unbeaten, kocha wa malengo, bado yupo sana Msimbazi. Kocha hajapoteza mechi, kocha ametupeleka Makundi, yupo Simba kutimiza malengo ya kuchukua ubingwa wa Ligi Kuu na malengo mengine ambayo tumempa," alisema Ahmed.


Kelele hizo za mashabiki ziliibuka kwenye mchezo dhidi ya Power Dynamos ambao Simba walifuzu kwa kupata sare ya goli 1-1 ambapo mashabiki hao hawakuridhishwa na kiwango cha wachezaji siku hiyo na kushinikiza kocha aondolewe.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad