Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amemaliza ziara yake ya Kitaifa ya siku tatu ya Nchini Zambia kwa mwaliko wa Rais wa nchi hio Hakainde Hichelema.
Akiwa Zambia, Rais Samia na Rais wa Zambia Mh. Hakainde wameshuhudia kusainiwa kwa Mikataba nane ya Ushirikiano wa Nchi hizo mbili.
Mikataba hiyo ni pamoja na
i). Hati ya Makubliano kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zambia kuhusu Mradi wa Usafirishaji Gesi Asilia kutoka Tanzania Kwenda Zambia.
ii). Hati ya Makubaliano kati ya Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania na Wakala wa Maendeleo Zambia.
iii. Hati ya Makubaliano kati ya Kituo cha Uwekezaji Tanzania na Wakala wa Maendeleo Zambia
iv. Hati ya Makubaliano ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania na Jamhuri ya Zambia katika Sayansi, Teknolojia na Ubunifu.
v. Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu programu ya kubadilishana Wanafunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu.
vi. Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu programu ya kubadilishana Wakufunzi wa Kozi ya Ukamanda na Unadhimu.
vii. Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu programu ya kubadilishana Wanafunzi wa Kozi ya Afisa-Cadet.
na
viii. Mkataba wa Utekelezaji kati ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Jeshi la Ulinzi la Zambia kuhusu ushirikiano katika Huduma za Tiba.