Hospitali ya Mloganzila Kuanza Kutoa Huduma za Kuongeza Shepu na Matiti
Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa mara ya kwanza nchini itafanya huduma za kibingwa bobezi za upasuaji wa kupunguza uzito na upasuaji rekebishi (Bariatric and Reconstructive surgery) ambao utahusisha kupunguza mafuta na kurekebisha sehemu ya mwili mfano kupunguza au kuongeza ukubwa wa matiti na makalio, kupunguza tumbo au nyama kwenye mikono na sehemu nyingine za mwili.
Mkuu wa Idara ya Upasuaji Dkt. Eric Muhumba amesema upasuaji huo utaanza kufanyika kuanzia October 27,2023 na utafanywa na Wataalamu wa MNH-Mloganzila kwa kushirikiana na Daktari Bingwa wa Upasuaji wa kupunguza uzito na Upasuaji Rekebishi kutoka India, Dkt. Mohit Bhandari pamoja na MedINCREDI.
“Upasuaji huu utafanyika kwa bei nafuu sana ukilinganisha na endapo Mtu angeenda kutafuta huduma hizi nje ya Nchi, hivyo tumeamua kuwasogezea Wananchi huduma hizi na kuwapunguzia usumbufu wa kusafiri nje ya Nchi kutafuta huduma hizi”