Idadi ya waliofariki ajali ya Vigwaza yaongezeka

 

Idadi ya waliofariki ajali ya Vigwaza yaongezeka

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, ACP Pius Lutumo amesema idadi ya waliofariki katika ajali ya Barabarani iliyosisha magari mawili kugongana uso kwa uso, imeongezeka na kufikia watu wanne kufuatia kifo cha mtu mmoja Kombora Rashidi Mbuma ambaye alikuwa akipatiwa matibabu Hospitalini ya Msoga, iliyopo Chalinze.


Amesema, majeruhi watatu wanaendelea vizuri na matibabu na kuwataja waliohamishiwa MOI kuwa ni Kaundime Juma Muyinga na mtoto wa mwaka mmoja Abdallah Ally ambaye anaendelea kupatiwa matibabu na afya yake ikiendelea kuhimarika, huku Amina Kondo (77), akiruhusiwa.


“Miili ya marehemu yote minne imekabidhiwa kwa ndugu zao kwa taratibu na hatua za mazishi na ikumbukwe ajali hiyo ilihusisha gari dogo aina ya Kluger lenye namba T.478 DCQ ikitokea Iringa kwenda Dar es Salaam likiwa na watu saba wa familia moja na Lori lenye namba T. 851 AQC aina ya Scania,” amesema Kamanda Lutumo.


Waliofariki katika ajali hiyo ni Dereva wa gari dogo, Maneno Mbuma anayekadiriwa kuwa na umri wa kati ya miaka 35-40, mwingine alifahamika kwa jina moja la Pokea (19), mkazi wa Mbezi Beach na Mwanahamisi (18), mkazi wa Kijitonyama, Dar es Salaam.


Ajali hiyo, ilitokea Oktoba 23, 2023 baada ya Dereva kujaribu kuyapita magari mengine bila ya tafadhari huko Kijiji cha Mbala, Kata ya Vigwaza Wilaya ya Bagamoyo Mkoa wa Pwani, ambapo Watu wa watatu wa familia moja walifariki dunia na majeruhi wawili wamehamishiwa MOI.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad