Israel yatangaza vita baada ya kupigwa makombora 5,000




Israel. Taifa la Israel limesema liko vitani baada ya kushambuliwa kwa makombora 5,000 na kundi la wanamgambo wa Hamas kutoka nchini Palestina. DW imeripoti.

Israel imetoa kauli hiyo ikiwa ni majibu ya shambulio hilo la kushtukiza lililotekelezwa jana Jumamosi Oktoba 7, 2023 ambapo kulingana na Shirika la France 24 waisraeli 232 wameuawa huku wengine zaidi ya 1500 wakijeruhiwa huko Gaza.

Inaelezwa wanamgambo wa Hamas walianza mashambulizi yao alfajiri ya jana Jumamosi kwa msururu wa makombora kuelekea kusini mwa Israel ambayo yameacha kilio katika nchi hiyo ya Mashariki ya Kati.

Shambulio hilo linatajwa kuwa baya zaidi kufanywa likiwa ni lakulipiza kisasi kwa jeshi la Israel. Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu amesema Hamas itawajibishwa vikali kwa kitendo hicho.

Wakati huohuo mamlaka za Israel zimewaonya watu wake wanaoishi karibu na maeneo ya ukanda wa Gaza ambao unadhibitiwa na Hamas kubaki ndani ya nyumba zao baada ya wanamgambo kadhaa kujipenyeza ndani ya nchi hiyo.

Mataifa mbalimbali duniani yakiwemo Marekani, Umoja wa Ulaya na jumuiya ya kujihami ya NATO zimelaani mashambulizi hayo ya Hamas, na kutangaza mshikamano kwa Israel na watu wake.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad