Kanye West Afuta Mipango ya Kugombea URAIS wa Marekani Mwaka 2024

 

Kanye West Afuta Mipango ya Kugombea URAIS wa Marekani Mwaka 2024

Mwanasheria wake ameliambia Jarida la #RollingStone kuwa Nyota huyo ameanza kufungasha vifaa vyote vilivyoandaliwa kwaajili ya Kampeni kwasababu hana tena mpango wa kuwania Urais tofauti na alivyotangaza awali

Kwa mujibu wa Mweka Hazina wa Kampeni za #YE24 Mfuko wa Kampeni umesalia na takriban Tsh. Milioni 62.5, kiasi ambacho hakiwezi kusaidia harakati hizo. Pia, Mweka hazina wa zamani wa West amesema kujaribu kushiriki Uchaguzi ni sawa na kuunda Ndege ambayo haina Mabawa na haitoweza kuruka

Katika Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2020, Kanye alipata Kura 60,000 katika Majimbo 12 kati ya Kura Milioni 239.9 zilizopigwa. Rapa huyo ambaye anapanga kuachia Albamu yake na Ty Dolla $ign, ametumiwa ujumbe na Bosi wa MayBach Music, Rick Ross, akimtaka ajiunge na 'Lebo' yake kutokana na kukosa Msambazaji wa Albamu hiyo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad