Kibu Denis Ndiyo Mbappe wetu Tanzania - Mchumbuzi Oscar Oscar

 

Kibu Denis Ndiyo Mbappe wetu Tanzania - Mchumbuzi Oscar Oscar

Wakati tunawapamba wachezaji wa kigeni pia tunapaswa kuwapamba wachezaji wazaw,bahati mbaya jana baada ya mechi ya Simba wadau wanazungumza ishu ya waamuzi badala ya ubora wa Kibu Dennis.


Wadau wa Soka wanasahau kuna kijana Mtanzania Kibu Dennis alipitia wakati mgumu wa kiwango chake kushuka,akaenda mapumziko nje ya nchi! Kibu angepotea ingefanya Taifa Stars tukose jembe la kwenda nalo AFCON.


Mechi ya jana tuachane na waamuzi na tuendelee kusifia ubora wa Kibu Dennis. "Rasta" jana alikuwa zaidi ya mchezaji wa kawaida,ile movement yake ya pembeni iliowafanya wakina Gadiel kulamba nyasi za uwanja wa Liti ni kitu cha kufunikwa na madudu ya waamuzi kweli?


Tuwe serious kidogo kwa wachezaji wa kikwetu pindi wanapofanya vizuri tuwape sifa na kuwaimba kama kina Clatous Chama,Zouzoua Pacome ama Max Nzengeli ambao kila siku wanasifiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad