Kifaa maalum cha kuzuia maambukizi ya UKIMWI chazinduliwa Afrika Kusini

 

Kifaa maalum cha kuzuia maambukizi ya UKIMWI chazinduliwa Afrika Kusini

Pete ya "mapinduzi" ya kuzuia HIV ambayo itavaliwa katika uke itazinduliwa hivi karibuni nchini Afrika Kusini – ambayo ina maambukizi mengi zaidi duniani, ushirika wa ufadhili wa kimataifa ulisema Ijumaa.


Mfuko wa Golobal Funds katika mapambano ya UKIMWI, Kifua Kikuu na Malaria ulisema vikundi vitatu vinavyohusika katika mapambano dhidi ya UKIMWI nchini vinaunga mkono jitihada hizo, vimeweka oda ya awali ya pete 16,000 -- ambazo zinatarajiwa kupatikana katika miezi ijayo.


"Tuna hakika kwamba pete hii mpya (pre-exposure prophylaxis) inaweza kuwa na matokeo ya kimapinduzi katika kuzuia VVU," alisema Peter Sands mkurugenzi mtendaji wa Global Fund.


Pete ya silicone, ambayo huvaliwa muda wote na kubadilishwa kila mwezi, hutoa dawa ya dapivirine inayorefusha maisha.


Utoaji wa awali utatumika kama hatua ya kwanza ya kuongeza upatikanaji wa matibabu na kuifanya pete ipatikane kwa urahisi katika nchi ambayo karibu watu milioni 8 wanaishi na VVU, kulingana na Mfuko wa Kimataifa.


Dawa za zinazo saidia kupunguza makali ya virusi,z inazuia kuwaambukiza wengine na pete hizo zimekuwa muhimu katika kuzuia kuenea kwa UKIMWI katika miongo kadhaa iliyopita.


Lakini kabla ya kuambukizwa, prophylaxis kwa kawaida hujumuisha kumeza kidonge kila siku au kuchomwa sindano kila mwezi -- njia ambazo hazifai kwa kila mtu, mashirika ya misaada ya UKIMWI yanasema.


"Wanawake wanahitaji kupata aina mbalimbali za njia salama na zinazofaa, ikiwa ni pamoja na pete ya dapivirine, ili waweze kuamua kutumia kile ambacho kinawafaa zaidi," alisema Ntombenhle Mkhize, Mkurugenzi Mtendaji wa taasisi ya UKIMWI wa Afrika Kusini.


Cha kusikitisha, ukijumuisha gharama na kunyimwa kisiasa, dawa za kuokoa maisha ambazo zilianza kutumika mwishoni mwa miaka ya 1990 hazikuweza kupatikana kwa Waafrika Kusini maskini na maelfu ya wagonjwa wa UKIMWI walikufa, kulingana na kadirio moja.


Leo, vifo vimepungua lakini maambukizo mapya bado ni mengi.


Mwaka huu, wanawake na wasichana wamechangia asilimia 53 ya maambukizo yote ya VVU duniani, kulingana na UNAIDS.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad