Kocha Cedric Kaze Hali Ngumu, Ajiuzulu Ukocha Namungo FC



Aliyekuwa Kocha wa Namungo FC, Cedric Kaze leo ametangaza kung’atuka kwenye nafasi hiyo akitoa taarifa kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.

Kaze ameandika “leo nimeamua kujiuzulu kama Kocha Mkuu wa Namungo, ningependa kutumia fursa hii kuushukuru uongozi, watendaji wenzangu wa benchi la ufundi na wachezaji kwa ushirikiano na kujitoa kwao”

Kaze pia amewashukuru mashabiki wa timu hiyo kwa ushirikiano wao.

Kaze hakuwa na matokeo mazuri kwenye mechi sita alizocheza ambapo jana alipoteza kwa mara nyingine baada ya kupokea kichapo kutoka kwa Singida FG.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad