Kocha Gamondi Akemea Ubinafsi Young Africans



Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Young Africans, Miguel Angel Gamondi, amewataka wachezaji wa timu hiyo kuacha kuangalia mambo binafsi haswa katika kushindania takwimu kwani jambo hilo litasababisha madhara makubwa ambayo hayatakuwa na msingi na tija ndani ya timu hiyo.

Gamondi amezungumza hayo kutokana na kuonekana wachezaji wake watatu ambao wanacheza katika eneo la kiungo kulingana kwenye idadi ya mabao ambao ni Maxi Nzengeli, Pacome Zouzoua na Stephane Aziz Ki.

Wachezaji hao wote watatu kwa pamoja wamefanikiwa kufunga mabao 9 kwenye Ligi Kuu Bara, ambapo kila mmoja akiwa amefunga mabao matatu.

Gamondi amesema kuwa anafurahi kuona wachezaji wake wakifunga mabao, lakini ametoa wito kwa wachezaji hao kucheza kwa faida ya kuisadia timu na si kuangalia mambo yao binfasi kwani itasabisha hasara kwa timu.

“Wachezaji wangu nimekuwa nikiwaeleza juu ya kuwaza kuisadia timu kwanza na wao baadae, hivyo nimekuwa nikiwasisitizia kama watakuwa wanataka kushindana wao kwa wao basi timu hii haitaweza kupata faida kubwa, najua wachezaji wanapotaka kila mmoja kutaka kuonesha kitu basi huo utasababisha uchoyo na hio ni mbaya.

“Nafurahi kwa kuwa viungo wangu wanacheza vizuri na wote wanafunga, lakini wanatakiwa kufahamu kuwa wanafanya haya kwa ajili ya timu kwanza na hayo mengine ni baadaye,” amesema kocha huyo kutoka nchini Argentina.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad