Kocha Robertinho Akiri Kufanya Makosa Kipindi Cha Kwanza, Mabadiliko Haya Muhimu Kufanya Mechi ya Mrudiano

Kocha Robertinho Akiri Kufanya Makosa Kipindi Cha Kwanza, Mabadiliko Haya Muhimu Kufanya Mechi ya Mrudiano

Kocha Robertinho Akiri Kufanya Makosa Kipindi Cha Kwanza, Mabadiliko Haya Muhimu Kufanya Mechi ya Mrudiano

KOCHA wa Simba, Roberto Oliveira ‘Robertinho’ wala hana presha na mchezo wa marudiano akiwatumia salamu Al Ahly kuwa wanakwenda kupambana, huku akipangua kikosi.

Simba ilitarajiwa kuondoka jana kwenda Misri kwa ajili ya mchezo wa marudiano wa African Football League dhidi ya Ahly ambao juzi walilazimisha sare ya mabao 2-2 kwenye Dimba la Mkapa.

Akizungumza na Mwanaspoti alisema wataendelea kucheza kwa nidhamu, lakini kichwani hawazi kujilinda.

Kocha huyo alisema Simba itashambulia kwa akili huku ikitaka kuwa na makali ya kumalizia vizuri. “Mimi siyo kocha wa kujilinda sijawahi kuwaza kucheza hivyo. Simba itacheza kwa nidhamu kubwa tukitambua ubora wa wapinzani wetu lakini tutawashambulia kwa akili,” alisema Robertinho.

“Tunaweza kuwa na mabadiliko machache ya jinsi ya upangaji wa timu lakini kitu muhimu tutaingia na akili kubwa kupigania heshima ya Simba.

“Kila mtu ameona mchezo wa jana (juzi). Kama tukiuanza kama tulivyoanza kipindi cha pili kuna kitu tutakitengeneza. Hakuna timu isiyofungika.”

“Kuna makosa tulifanya kipindi cha kwanza. Kuna wakati tulitengeneza urahisi wa Ahly kutushambulia bila sababu za msingi. Nafahamu tulipambana na timu kubwa yenye wachezaji bora lakini tutabadilika.”

Robertinho alikiri kwamba anaweza kuwa na mabadiliko ya kikosi katika mchezo huo utakaopigwa Oktoba 24, jijini Cairo nchini. Simba inatakiwa kushinda mchezo huo ili iweze kutinga hatua ya nusu fainali.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad