Kocha wa SIMBA Robertinho akiri mabeki wake wana shida
Benchi la ufundi la Wekundu wa Msimbazi Simba limekiri kuwa na kazi ya ziada kurekebisha safu yake ulinzi, kuelekea katika mchezo wa Mzunguuko wa nane wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Mabingwa watetezi Young Africans.
Pamoja na kuwa Simba SC haijapoteza michezo yote 12 ya mashindano yote waliyocheza msimu huu, lakini safu yake ya ulinzi imeonekana kuwa na makosa mengi ya kiufundi ikifungwa jumla ya mabao 11, ikiwa ni karibu wastani wa bao moja katika kila mchezo jambo ambalo sio salama kwao.
Katika Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba SC imeruhusu mabao sita, matatu kwenye Ligi ya Mabingwa Barani Afrika na matatu katika michuano mipya ya African Football League.
Katika mechi zote hizo, muda ambao timu inaruhusu mabao hayo ukuta wa Simba SC umekuwa ukiundwa na wachezaji saba ambao ni mabeki watano, Henock Inonga, Che Malone, Kennedy Juma, Mohamed Hussein, Shomari Kapombe na makipa Ally Salim na Ayoub Lakred.
Kocha mkuu wa Simba, Roberto Oliveira amekiri ni makosa yanayojirudia lakini anaendelea kuyafanyia kazi kwa kuongea na kuwaelekeza wachezaji wake namna ya kuyapunguza.
“Ni kweli tumekuwa tukiruhusu mabao, jambo ambalo hatulifurahii na siyo zuri kwetu.
Try Again: Ihefu FC imetupa mazoezi ya Dabi “Kila siku mazoezini tumekuwa tukilifanyia kazi lakini linajirudia. Kwa sasa tuna muda kidogo kabla ya mchezo wetu ujao, tutajitahidi kulifanyia kazi eneo hilo ili kuhakikisha makosa hayo yanapungua,” amesema Robertinho na kuongeza;
“Ni makosa madogo madogo wanafanya wachezaji ila pamoja na kukosea huko, wamekuwa wakifanya kazi kubwa kuhakikisha tunakuwa salama, nadhani sio wakati wa kuwabeza kwani wana mazuri mengi kuliko mabaya.”
Kwa upande Beki wa zamani wa Simba SC, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, alisema kila timu inafungwa na kila mchezaji anafanya makosa hivyo kinachotakiwa ni kuangalia namna ya kuyapunguza makosa hayo.
“Mabeki wa Simba wote kila mmoja anasifa zake kwa hiyo kinachotakiwa ni kuwafanya waelewane zaidi katika upungufu na uimara wao ili kupunguza makosa,” amesema Julio.
Simba SC na Young Africans zitakutana zote ziikiwa na alama 18, huku Young Africans ikiongoza kwa tofauti ya mabao 16 kwa 11 ya Simba SC