Kuelekea Super League, Mpango wa Mbrazili SIMBA Kumaliziana na Al Ahly Uko Hivi

 

Kuelekea Super League, Mpango wa Mbrazili SIMBA Kumaliziana na Al Ahly Uko Hivi

Kuelekea Super League, Mpango wa Mbrazili SIMBA Kumaliziana na Al Ahly Uko Hivi

Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ ana jambo lake ndani ya timu hiyo kwani imefichuka ameagiza benchi lake la ufundi kutumia michezo yao ya Ligi Kuu Bara kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wao wa Robo Fainali ya African Football League dhidi ya Al Ahly.

Simba SC wanatarajiwa kuvaana na Al Ahly katika mchezo wa mkondo wa kwanza wa Robo Fainali ya African Football League ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam wakiwa ndiyo wawakilishi pekee wa Tanzania katika mashindano hayo mapya.

Kuelekea mchezo huo Simba SC watakuwa na michezo miwili ya Ligi Kuu Bara ambapo mchezo wa kwanza ulipigwa jana Alhamisi (Oktoba 05) dhidi ya Prisons kabla ya kuvaana na Singida Fountain Gate Jumapili ya keshokutwa.

Robertinho amesema: “Ni wazi kama timu tuna ratiba ngumu katika siku chache zijazo ambapo tumecheza na Tanzania Prisons, na sasa tunakwenda kucheza na Singida Fountain Gate FC kabla ya kuanza majukumu ya mashindano ya African Football League.

“Hivyo ni wazi hatuna muda wa kupoteza tunatumia michezo ya ligi kama sehemu ya maandalizi yetu kuelekea michuano hiyo mipya mikubwa na muhimu.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad