Inaripotiwa kuwa, ili Kylian Mbappe aweze kufanikisha uhamisho wake kwenda, Real Madrid, basi atalazimika kukata uhusiano wa kikazi na mama yake, Fayza Lamari ambaye amekuwa akimsimamia kama wakala wake.
Uamuzi huo hauepukiki sababu sheria mpya ya FIFA inaelekeza kwamba, ni mawakala wenye leseni tu, ndio wanaoruhusiwa kujadili uhamisho na mikataba ya wachezaji.
Fayza Lamari, hatambuliki na Shirikisho la Soka Ulimwenguni, (FIFA) kama wakala, hivyo inamuwia vigumu kumuwakilisha mchezaji yeyote kwenye matukio rasmi.
Pia hakuna ushahidi kama Lamari, alifanya mtihani wa kupata vyeti husika, baada ya kukosekana jina lake kwenye orodha ya mawakala wanaotambulika na FIFA.
Vile vile, ni ngumu kwa Lamari kupata vyeti husika kabla ya Mei 2024, na anakabiliwa na hatari ya kupigwa faini ikiwa ataendelea kumwakilisha mwanawe.
kwa hivyo ili Mbappé, afanikishe uhamisho wake kwenda Real Madrid au kuongeza mkataba na PSG, basi atalazimika kutafuta wakala mwingine.