Mabosi wa Simba Wafunguka: Hatuwadai kitu Wachezaji Wetu Wamepambana Kijemedari




LICHA ya Klabu ya Simba kuwa na vizingiti vya kutinga hatua ya nusu fainali katika michuano ya kimataifa, uongozi umewapongeza wachezaji namna walivyopambana ugenini na kutoka sare ya bao 1-1.

Simba juzi ilikuwa mgeni wa Al Ahly katika mchezo wa marudiano wa African Football League uliochezwa Cairo, Misri na kuambulia sare iliyoitoa kwenye mashindano baada ya nyumbani kufungana mabao 2-2.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Klabu ya Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’ alisema walitolewa kimchezo, lakini wao kama viongozi hawana deni na mastaa wao kutokana na ubora waliouonyesha.

Alisema wachezaji walipambana kwa jasho jingi, lakini bahati haikuwa upande wao walitolewa katika mashindano, hivyo wanajipanga kwa ajlili ya michezo ijayo siku za usoni ili waweze kufanya vizuri.

“Wachezaji wamecheza, wameonyesha ukubwa wao katika michuano mkubwa inayowakutanisha wakubwa hatuna tunachowadai wamepigana sana ilitakiwa mshindi apatikane ndio matokeo ya mpira,” alisema Try Again.

Mwenyekiti huyo alilipongeza benchi la ufundi kwa namna ambavyo linazidi kukiimarisha kikosi hicho na kuendelea kuwa bora kila siku.

“Benchi letu la ufundi ni zuri na tunaliamini lina watu bora na sahihi katika kutufikisha kwenye malengo yetu ambayo tumejipanga kuyafikia,” alisema.


Simba imekuwa na wakati mgumu wa kunusa nusu fainali na kujikuta ikikwama robo fainali mfupa ambao umewashinda na wanatakiwa kupambana kuuvunja, ikiwa mara tatu wameishia robo fainali michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad