Majaliwa Jackson Kijana Aliyeokoa Watu Kwenye Ajali ya Ndege Precision Air Akanusha Kutelekeza Mtoto na Kuidanganya Serikali

 


Majaliwa Jackson Joseph, kijana aliyesaidia kuokolewa kwa Watu 24 katika ajali ya ndege ya Precision Air iliyotokea Ziwa Victoria November 6 mwaka jana amesema kila alichokisimulia baada ya tukio la uokoaji kilikuwa cha kweli na hakuidanganya Serikali wala Watanzania huku pia akikanusha madai ya kwamba alitelekeza Mtoto na kusema hana Mpenzi wala Mke kwa sasa lakini akiamua kuwa nae atazingatia kigezo cha Mke Mcha Mungu.


Mwandishi wa @AyoTV_, Bakari Chijumba amefika Visiwani Zanzibar, na kuongea na Majaliwa baada ya kuhitimu mafunzo yake ya Zimamoto na Uokoaji katika Chuo cha KMKM ambapo amesema “Unajua siku zote Mungu akikuvusha kutoka daraja moja kwenda jingine maneno hayawezi kukosekana utaambiwa vingi”


“Unajua Watanzania sisi au Binadamu tuna nature ya kubeza vitu, Mimi mpaka hapa nilipo ni uwezo wa Mungu, Mungu ndio anapanga riziki ya Mtu, maneno yanayoendelea mtandaoni siwezi kuwazuia wasiongee, Mimi sio muongo halafu Mimi ni Kijana mdogo huwezi ukatoka hapa unakuja kuidanganya Serikali wewe ni nani?, Tanzania kuna Watu Mamilioni halafu Kijana Mimi ndio kwanza nina umri wa miaka 22, 23 siwezi kuwadanganya”


“Namshukuru sana Mungu ni kitu kinanipa faraja kutoka nilipokuwa hadi sasa naweza kuwa Mwalimu wa kuwafundisha Watu kuogelea na kupiga mbizi, namshukuru Rais Dkt.Samia kwa upendo wake amenifanya kama Mwanae, nimelelewa na Mzazi mmoja (Mama) na Baba anajua lakini kwa wake huohuo mdogo namwambia nampenda sana na nitamsaidia, Wavuvi wenzangu wasijali hichohicho kidogo tutashare maana tumetoka mbali, napenda nyimbo za Utu ya Kiba, Dungamawe ya Kontawa na Mkuki moyoni ya Afande Sele”


Video nzima kuhusu yote aliyoyasema Majaliwa kuhusu maisha yake tayari ipo kwenye Youtube ya millardayo

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad