Majeruhi Ajali ya Moto Kariakoo ni Watano


 Majeruhi Ajali ya Moto Kariakoo ni Watano

Baada ya maafa ya moto uliyozuka jana Oktoba Mosi, 2023 Kariakoo katika eneo la Mnadani Auction Mart, Jeshi la Zimamoto limetangaza majeruhi wa tano akiwemo mtoto mmoja na wengine wanne ambao waliwahishwa hospitalini.


Hayo yamesemwa leo Septemba 2, 2023 na kamanda wa jeshi la zima moto na uwokoaji kamishna msaidizi mwandamizi Christina Sunga akizungmza nasi.


Ameeleza changamoto walizokutana nazo kama jeshi la ukoaji na zima moto jinsi gani miundombinu hafifu imesababisha baadhi ya maeneo kutofikiwa kwa wakati na kusababisha moto kuendelea kusambaa.


“Lakini kama mnavyoona eneo hili lilikuwa katikati ya majengo ambapo njia za kupitia hazikuwa kubwa kuruhusu gari la zima moto kuingia hivyo ikaleta changamoto kubwa na uchelewaji wa kupambana na moto ambao ulikuwa ukiwaka kwenye eneo hili la soko la mnadani.”


Aidha tathmini ya hasara zilizopatikana inaendelea kufanywa kushirikiana na uongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad