Malori Zaidi Ya 250 Ya Tanzania Yakamatwa Congo DRC, Wamiliki Waililia Serikali





Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Malori nchini (TAMSTOA), Chuki Shabani akizungumza na wanahabari (hawapo pichani).
Malori zaidi 250 yaliyokuwa yamebeba madini kutoka Congo DRC yanadaiwa kukamatwa nchini humo kwa kile ilichoelezwa ni mgogoro wa ulipaji kodi kati ya wawekezaji wa machimbo ya madini na serikali ya nchi hiyo.

Akizungumza na wanahabari jijini Dar Mwenyekiti wa Chama Cha Wamiliki wa Malori nchini (TAMSTOA), Chuki Shabani amesema malori hayo tangu yakamatwe mpaka jana (Jumanne) ilikuwa yameshafikisha siku arobaini.


Mkutano wa wamiliki wa malori nchini, ukiendelea.
Mwenyekiti huyo akizungumza na wanahabari amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan na serikali kwa ujumla kuingilia kati suala hilo ili magari yao yaachiwe ikiwekana yakafanye shughuli zake sehemu zingine kwakuwa mgogoro huo wa kodi wao hauwahusu.

Chuki Shabani amemuomba Rais Samia kuwasaidia kama alivyowasaidia malori yao yaliyopakia magogo yalipozuiliwa nchini Zambia na kuongeza;


Sehemu ya wamiliki wa malori wakizungumza na vyombo vya habari.
“Mama yetu mpendwa, Rais wetu Dk Samia Suluhu Hassan tunaomba utusaidie kwa mara nyingine usituchoke, maana wananchi wako tunanyanyasika kwa makosa yasiyotuhusu.

“Mbaya zaidi yamekamatwa malori yote yaliyoingia eneo la mgodi hata yale ambayo bado hayajapakia mzigo na madereva kutelekezwa eneo la Kasumbalesa ambalo halina huduma za kijamii kama vile maji, vyoo, huduma za afya, ulinzi wao na mali zao nakadharika.” Alimaliza kusema Chuki. HABARI/PICHA: RICHARD BUKOS NA ISSA MNALLY /GPL 

Tags

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad