Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Yapiga Marufuku Matumizi Holela ya VPN

 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Yapiga Marufuku Matumizi Holela ya VPN

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) imesema imebaini upatikanaji wa maudhui yaliyokatazwa kwa kupitia matumizi ya mtandao binafsi (VPN) kinyume cha kanuni hivyo imetoa taarifa kwa Umma, Watu binafsi na Makampuni ambayo kwa asili ya majukumu na kazi zao, matumizi ya mtandao binafsi (VPN) hayazuiliki, kutoa taarifa kwa TCRA juu ya VPN wanazotumia na taarifa zote muhimu ikiwemo anuani ya itifaki ya mtandao (IP Address) kabla au mnamo October 30, 2023 kupitia tcra.go.tz.


“TCRA itaendelea kuchukua hatua za kiudhibiti dhidi ya matumizi ya mtandao binafsi (VPN) yasiyo halali ikiwemo kuzuia upatikanaji wa VPN ambazo hazijatolewa taarifa au kusajiliwa.


“TCRA inapenda kuukumbusha Umma kuwa, utoaji, umiliki au usambazaji wa teknolojia, programu, programu tumizi au kitu chochote kinachoendana na ambacho kinaruhusu au kumsaidia mtumiaji kupata maudhui yaliyokatazwa ni kosa la jinai, linaloadhibiwa baada ya kutiwa hatiani, kwa faini ya shilingi za Kitanzania zisizopungua milioni tano au kifungo kisichopungua miezi kumi na mbili au vyote kwa pamoja.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad