Manara: Waacheni Mashabiki Wamzomee Fei Toto

Manara: Waacheni Mashabiki Wamzomee Fei Toto

 Manara: Waacheni Mashabiki Wamzomee Fei Toto

Nimeona baadhi ya Wachambuzi wanawalaumu Washabiki wetu kumzomea uwanjani @feisal194 jana na wanasema haikuwa sahihi.


Kwangu ilikuwa sahihi 100%,kazi kuu ya Mshabiki ndani ya Uwanja ni kushangilia na kuzomea, hawaendi kuuza sura wala kukata mabuno pale Stadium, nyie Wachambuzi wengi wenu ndio mliokuwa mnaandika makala nyingi za kumchochea Fesal asiondoke vizuri Yanga na yeye akajaa katika mfumo wenu, What do you expect ?


Kutwa ilikuwa mitandaoni kumejaa mipasho na rufaa za kila sampuli!! Ukitaka kuamini hilo Mbona @ybangala4 hajazomewa? Sababu kaondoka bila mipasho pasho yenu ,,kaomdoka kimya kimya na bila maneno ya kukerana!!


Yaani fesal mlitegemea jana ashangiliwe baada ya zogo lote kuhusu usajili wake? Mmerogwa?


Hawamchukii hata kidogo na ndio maana hajawahi kuzomewa mtaani, lakini ndani ya Pitch kuzomewa ni Wajibu, hayo ndio matakwa ya football!!


Washabiki wa Team za mpira wanapenda Team zao hawapendi Mtu, Fesal mdogo wangu usikubali uchonganishi huo tena, hiyo ndio kazi ya Wanazi wa Soka, Wanakujaza tena hao uwaone @yangasc wanakuchukia mno, narudia hyo ndio kazi yao kuu, utazomewa sana game dhidi yao hadi hasira ( mapenzi na ww) yatakapoisha!!


Angalia mimi kaka yako Washabiki wa kikolo wanavyonizodoa huku mitandaoni,hata Mange aliandika negative kuhusu mimi wanafurahi, unadhani wananichukia? Ni hasira tu za mimi kuondoka kwao, lakini nikikutana nao kitaa wanaomba selfie.


Shida ya Wachambuzi wengi hawana wajualo kuhusu Football na tamaduni zake ,ni wafata mkumbo waliokutana na Kandanda uzeeni, na walishajiandaa na makala zao za kukusifu, sasa zimebuma, hasira zao wamehamishia kwa Washabiki wa Mabingwa wa Nchi!!


Imagine washaanza kusema eti Why huitwi Team ya Taifa? Yes performance yako ya jana ya kukamia mechi was superb, je uitwe team ya taifa kwa mech moja? Wape consistency, fanya hivyo tena na tena tuone kama hutakwenda Abidjan.


Nb: Makolo leo mle mapema kisha mshibe hasa, tena ndi ndi ndi, muda wa maafa unazidi kusogea

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad