Mbunge Byabato Apiga Magoti Machozi yakimlenga Lenga

Mbunge Byabato Apiga Magoti Machozi yakimlenga Lenga


Mbunge wa Jimbo la Bukoba Mjini ambaye pia ni Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia Afrika Mashariki Stephen Byabato, amekutana na kuongea na Wananchi wa Jimbo la Bukoba Mjini katika hafla ya kukabidhi mkataba kwa Mkandarasi wa ujenzi wa Stendi ya Kisasa ya Bukoba.


Kupitia hafla hiyo amelazimika kupiga magoti huku akilengwa na machozi akiwaomba baadhi ya Wananchi kuacha kumukwamisha wakati anapopigania shughuli za kuleta maendeleo kwa Wananchi.


“Bukoba hii ni ya kwetu sisi tukitaka kuiharibu tutaiharibu, nawaomba tusaidiane kusogeza Bukoba yetu mbele tusikwamishane, mmenipa miaka mitano mnisaidie niikamilishe lakini ninachowaahidi sitoacha kufanya eti kisa nitakosa Ubunge, haki ya Mungu siachi nitafanya kama ni Ubunge mchukue ila miradi ya Bukoba muiache itekelezwe, sote hatuwezi kuwa Wabunge, sasa kupambana kwa ajili ya Wana Bukoba kwanini iwe nongwa, naomba mnisaidie”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad