MSHAMBULIAJI kinda wa Yanga, Clement Mzize mwenye mabao matano katika michuano yote hadi sasa amefichua mambo mawili yanayombeba kwenye kiwango chake msimu huu ndani ya timu yake.
.
Amesema jambo la kwanza ambalo limemuongezea ubora ni mafunzo na maelekezo anayoyapata kwa kocha wao msaidizi Mussa Nd’aw ambaye ni mshambuliaji wa hatari wa zamani wa Kimataifa wa zamani, ambaye enzi zake alichezea klabu nyingi ikiwemo Wydad Casablanca ya Morocco, Al-Hilal ya Saudà Arabia, Farense ya Ureno na Al Ittifaq.
.
“Amekuwa akinijenga sana, ni kocha ambaye ana vitu vingi bahati nzuri na yeye alicheza nafasi kama yangu tena kwa mafanikio makubwa kila wakati amekuwa akinikosoa na kunielekeza cha kufanya,” alisema Mzize.“
.
Mzize ameongeza kuwa mbali na mafunzo hayo kutoka kwa kocha wake pia amekuwa na ratiba binafsi ya kufunga wanapomaliza mazoezi ya timu nzima au kabla.