Mchezaji Max Azawadi Gari Jipya na Mabosi wake


YANGA iko kambini kwaajili ya maandalizi ya kukutana na watani wao wa jadi Simba, kiungo wao Maxi Nzengeli amepata mzuka wa aina yake haswa kutokana na kiwango chake cha sasa huku akisema mechi ya Jumapili itanoga.

Mabosi wa Yanga mara baada ya kiungo huyo kupiga mabao mawili kwenye ushindi wa 2-0 dhidi ya Singida Big Stars wakamfanyia jambo kwa kumpa zawadi ya Gari ili kumpandisha mzuka zaidi wa dabi.
Maxi kuanzia juzi anatembelea gari hiyo aina ya Toyota Crown iliyotolewa na mabosi wa klabu hiyo kwa kiwango ambacho amekiendelea kukionyesha huku ikielezwa kuwa pia ilikuwa ni sehemu ya makubaliano ya pande hizo mbili.

Amezungumzia mechi dhidi ya Simba na kusema ni miongoni mwa mchezo wenye presha na mgumu kwani zinakutana timu kubwa zenye ushindani na ubora hivyo macho ya watu yanatamani kuona nini kitakwenda kutokea na wao wamejipanga kufanya jambo.

“Huu ni mchezo mkubwa utakaotazamwa sana hivyo kila mchezaji anatakiwa kucheza kwa juhudi kubwa na morali ili kuweza kufanikiwa katika mechi hiyo yenye ushindani mkubwa,”alisema Maxi huku akionyesha kuwa na ari ya mchezo huo ambao Simba ni wenyeji.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad