Mchezaji Maxi Nzengeli ni BORA Kuliko Clatous Chama?
Siku za hivi karibuni kumekuwa na mijadala mingi sana mitandaoni kuhusu ubora wa viungo wawili wanaotesa sana kwenye Ligi kuu ya NBC, moja ni kutoka Congo Max Nzengeli “Mbappe wa Congo” na Clatous Chama “Mwamba wa Lusaka.”
Viungo hawa wawili ni msaada mkubwa kwenye timu zao kwani mpaka sasa kila mmoja amehusika kwenye ushindi wa timu yake, na wote wanacheza eneo moja la kiungo kama wachezeshaji “Play Maker”
Mjadala uliopo ni kwamba Max Nzengeli ni bora kuliko Chama, huenda wanaovutia kamba kwao wanamashiko kwa sababu ya takwimu nzuri za mchezaji huyo kwenye timu yake sasa, mfano mchezo dhidi ya Geita Gold amefunga bao moja na kutoa asisti 1 hivyo kuhusika kwenye mabao 2.
Vile vile kwa Chama na Simba yake ambapo kwa muda mrefu Mwamba amekuwa akifanya mambo makubwa na kulinganishwa na mastaa kibao wanapofika Tanzania akiwemo Aziz Ki, Paccome, Harouna Niyonzima na sasa Max Nzengeli. Lakini Chama ataendelea kubaki kwenye dunia yake na hao wengine watabaki kwenye dunia yao.
Ni mapema sana kuanza kuweka mijadala ya ubora wa wachezaji kwa mechi 4 tu za Ligi, tena mchezaji mpya ambaye hajamaliza hata msimu mmoja wa kimashindano, hivyo tuvute subira mpaka mwisho wa msimu takwimu zitaonekana.
Una maoni kuhusiana na mjadala huu? au unadhani nani kati yao ni Bora kuliko mwezake?