Mchezaji wa zamani wa Yanga Princess na timu ya taifa, Clara Luvanga ameingia mkataba wa miaka mitatu na timu ya soka ya wanawake ya Al Nassr kutoka Saudi Arabia
Ni miezi miwili tu imepita baada ya kusajiliwa na Dux Lugrono ya Hispania na miamba hiyo ya soka ya Saudia kuvunja mkataba wake na timu hiyo
Clara alianza vyema kwenye Ligi ya Hispania na kuifungia timu yake bao moja iliposhinda mabao 7-0 na huenda Nassr walivutiwa na kiwango alichoonyesha straika huyo
Mtu wa karibu wa mchezaji huyo amebanisha kuwa bado kukamilisha taratibu za kiafaya na ikikamilika muda wowote Clara atatambulishwa
"Mwanzo ilikuwa England, Saudia na Sweden ndio zilikuwa zinamuhitaji lakini tuliangalia pesa ndefu bado kuna vitu vidogo kukamilika na muda wowote mambo yatakuwa safi," amesema mtu huyo
Kwa mkataba huo utamfanya Clara anunuliwe kwa Sh250 milioni na kuingiza mshahara wa zaidi ya milioni 16 kwa mwezi