Mechi ya Simba Vs Tanzania Prisons, Vikosi na Matokeo


TANZANIA PRISONS V/s SIMBA mechi hii haijawahi kuwa rahisi hususan inapochezwa uwanja wa Sokoine, Mbeya! Historia inaonesha timu hizi zinapokutana Mbeya kuanzia viongozi, benchi la ufundi na wachezaji wa Simba wanajua shughuli ipo.

Hata kama Simba inashinda basi mechi humalizika kwa ushindi wa 1-0, 2-1 na ikitokea imefunga magoli matatu basi ndio Tanzania Prisons imefungwa magoli mengi sana.

Kwa hiyo Tanzania Prisons kisaikolojia wanakuwa vizuri sana kwa sababu wanaamini hata kama wapo 'unga' kiasi gani wanaweza kupambana na Simba na wakapata chochote.

Kwa maana hiyo presha bado ipo kwa Simba na makocha huwa wanapewa hizo historia na kupewa takwimu za mechi zilizopita na kuambiwa kuwa ni miongoni mwa mechi ambazo wakati mwingine zinatibua mbio za ubingwa.

Ni mechi ngumu pia kwa Tanzania Prisons kwa sababu Simba wanajua kama leo watapata ushindi utaleta ahueni kwa benchi la ufundi na wachezaji kutoka kwenye presha ya mashabiki na mitandao.

Tanzania Prisons ndio timu pekee ambayo yenye alama moja kwenye msimamo wa Ligi huku ikiwa imecheza mechi tatu, haijashinda mchezo wowote, imetoka sare mchezo mmoja na kupoteza michezo miwili. Ndio timu ya mwisho kwenye msimamo, lakini ikipata alama tatu leo itafikisha alama nne na kusogea hadi nafasi ya 12.

Simba ina alama tisa baada ya kushinda mechi zote tatu zilizopita, endapo itashinda leo dhidi ya Prisons itafikisha alama 12 na kuongoza Ligi ikiitoa Azam FC ambayo inaongoza kwa sasa ikiwa na alama 10 baada ya kucheza michezo minne.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad