Mhubiri Ng’ang’a Ashangaza Watu Kwa Kukataa Sadaka ya Ksh 500




MCHUNGAJI tata wa Kanisa la Neno, James Maina Ng’ang’a amewaacha wengi kwa mshangao baada ya kukataa sadaka ya Sh500.

Kwenye video iliyochapishwa mtandoni, Ng’ang’a alionekana kukasirishwa na muumini mmoja aliyempa sadaka ya Sh500 na kumuomba akumbuke jamii yake nzima kwenye maombi.

Ng’ang’a, mchungaji huyo mahiri alijibu, “Mia tano hata nitawakumbuka namna gani sasa, hata hakuna mafuta ya gari ya mia tano labda pikipiki. Hiyo ni ibada gani sasa? Hiyo ibada ya mia tano fanya na waganga ambao wako Nairobi wale wa toa mbegu.”

Jibu lake pasta Ng’ang’a liliwakera wengi ambao walielekeza ghadhabu zao mitandaoni wakimkashifu kwa kutopokea kidogo alichopewa.

Walisema; “Na bado watu wanajazana kanisa lake. Unapaswa kutoa matoleo kulingana na moyo wako sio ili uoneshane,” akaandika Eric Samuel.

“Biashara lazima,” akasema David Mwamburi.

“Hii ndio sababu niliwacha kuenda kanisani,” akakiri Levi Mwanawassa.

“Kanisa ni biashara,” akaandika Stella Wavish.


Cha kushangaza ni kwamba, wiki jana, Pasta Ng’ang’a aliungana na Wakenya kulalamikia uchumi ulivyozorota na hata hali ngumu ya maisha.

Akizungumza katika ibada kanisani mwake, Ng’ang’a alieleza wakuu serikalini kuwa walikuwa wakiwalaghai Wakenya.

Alisema, “Naongea kama mtume. Uchumi ni mbaya na mnatumia hizo pesa vile mnataka. Mnapandisha uchumi huku, mnaongezea pesa huku, na mtu akiwaambia mnafunga kanisa. Si mkuje mfunge hii yangu! Kujeni mfunge!”

Akothee atishia kuzua fujo kwenye benki baada ya pesa zake...
Mwanakontenti Maureen amsifia aliyekuwa mumewe kwa kufungua...

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad