Miili ya baadhi ya Waisraeli walionaswa na Hamas wakati wa shambulizi lake wiki moja iliyopita imepatikana na jeshi la Israel wakati wa shambulio la ardhini huko Gaza siku ya Ijumaa, magazeti ya Israel yanaripoti.
Haaretz na Kituo cha Yerusalemu wanasema kuwa Jeshi la Ulinzi la Israeli lilipata idadi isiyojulikana ya miili, na kuirudisha katika eneo la Israeli, na kukuta baadhi ya vitu vya watu havipo.
Vikosi vya askari wa miguu na wenye silaha vilishiriki katika uvamizi huo ambapo seli ya Hamas ambayo ilirusha makombora ya vifaru katika eneo la Israeli "ilitolewa", gazeti la Jerusalem Post linasema.
"Hali ngumu zaidi ya utekaji nyara ambayo Israeli imewahi kukumbana nayo"
Takriban mateka 150 waliokamatwa na watu wenye silaha wa Hamas kutoka kusini mwa Israel Jumamosi iliyopita wanaaminika kushikiliwa katika maeneo ya siri ndani ya Gaza.Miongoni mwao ni wanawake, watoto na wazee.
Hamas ilikuwa imetishia kumuua mateka mmoja kwa kila wakati mashambulizi ya anga ya Israel yakiua raia bila ya onyo.Vyombo vya habari vya Israel vinaripoti kuwa wanajeshi waliokuwa wakivamia Gaza walipata miili na mali za baadhi ya watu waliotoweka.
Hili linaiacha serikali ya Israel na mtanziko.Je, inajaribu misheni ya uokoaji kwa kutumia silaha, kitu kilichojaa hatari?Au inasubiri kwa muda mrefu zaidi, hadi Hamas itadhoofishwa na mashambulizi ya anga kiasi kwamba inaweza kuwa tayari zaidi kufanya makubaliano?
Michael Milstein, ambaye alihudumu miaka 20 katika ujasusi wa kijeshi wa Israeli,alimwambia mwandishi wa usalama wa BBC Frank Gardner: "Hii ndiyo hali ngumu zaidi ya utekaji nyara ambayo Israeli imewahi kukumbana nayo katika historia yake