Mitihani Darasa la Nne na Form Two Kufutwa Zanzibar


Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar, Lela Mohammed Mussa leo October 18,2023 ametangaza baadhi ya mabadiliko na mageuzi ya elimu ikiwemo sera na sheria mpya ambazo zitatarajiwa kuendana na mabadiliko hayo kwa Zanzibar yanayotarajiwa kuanza kwa Wanafunzi waliopo madarasa ya chini kuanzia darasa la kwanza, mabadiliko hayo ni pamoja na kufuta mitihani ya darasa la nne na kidato cha pili.

"Serikali itaondoa mitihani ya Taifa ya darasa la nne na mitihani ya kidato cha pili, Serikali imeamua kufuta hii mitihani, kwanza sio kwamba inamfanya Mwanafunzi ahitimu au inamfanya Mwanafunzi asiendelee kusoma lengo la mitihani ni kumpima kafaulu au hakufaulu, tutaandaa utaratibu mwingine mzuri”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad