Mji wa Jerusalem umeshambuliwa na Hamas?? ving’ora vya mabomu vyasikika



Jeshi la Ulinzi la Israel linasema ving’ora vya mashambulizi ya anga sasa vinasikika mjini Jerusalem na kote Israel, huku makombora yakirushwa kutoka Gaza. Takriban milipuko mitatu imesikika huko Jerusalem.

Bado haijabainika iwapo hizi ni roketi zinazotua, au kunaswa na ulinzi wa Israel.

Wakati huo huo msemaji wa Jeshi la Ulinzi la Israel Daniel Hagari anasema jeshi limekomboa makazi yote karibu na kizuizi cha Gaza – lakini mapigano yanaendelea kati yao na wapiganaji wa Kipalestina.

Hapo awali, jeshi lilisema mapigano yalikuwa yakifanyika katika maeneo “saba au nane” ndani ya ardhi ya Israel.


Aidha Waziri wa Ulinzi wa Israel Yoav Gallant anasema ameamuru “kuzingirwa kabisa” kwa Ukanda wa Gaza: “Hakuna umeme, hakuna chakula, hakuna mafuta.”

Israeli kwa sasa inadhibiti anga ya Gaza na ufuo wake, na kuzuia ni nani na bidhaa gani zinazoruhusiwa kuingia na kutoka kupitia vivuko vya mpaka wake.

Vile vile, Misri inadhibiti wanaopita na kutoka katika mpaka wake na Gaza.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad