Mlipuko Kwenye Hospitali Ya Gaza Unamsababisha Biden Kuahirisha Ziara Ya Jordan

Mlipuko Kwenye Hospitali Ya Gaza Unamsababisha Biden Kuahirisha Ziara Ya Jordan


Rais Biden ameahirisha ziara yake ya Jordan akiwa njiani kuelekea Israel, baada ya mlipuko mkubwa kutokea kwenye hospitali moja mji wa Gaza City na kusababisha vifo vya mamia ya watu.


Rais Biden akiwa njiani kuelekea Mashariki ya Kati kujaribu kutafuta suluhisho la kusitisha ghasia zinazoendelea kati ya Israel na Hamas, ndipo serikali ya Jordan ilipotangaza kwamba mkutano wa kilele ulopangwa kufanyika Jumatano kati yake na viongozi wenzake wa Jordan, Misri na Palestina umeahirishwa.


Uwamuzi huo ulichukuliwa baada ya rais Mahamoud Abass wa Palestina kuamua kuondoka Amann ambako alipanga kuhudhuria mkutano huo akiwa amekasirishwa na shambulio dhidi ya hospitali inayosimamiwa na kanisa la batist mjini Gaza, la Al-Ahli Arab.


Kila upande katika vita hivyo vya Ukingo wa Gaza unamlaumu mwengine kwa mlipuko huo mkubwa ulotikisha hospitali ya Al-Ahli Arab, kwenye mji wa Gaza City na kusababisha vifo vya mamia ya watu.


Kundi la wanamgambo la Hamas kwenye taarifa Jumanne usiku, linailaumu Israel kwa shambulio dhidi ya hospitali hiyo, kikidai kwamba mamia ya watu walouliwa walikua wamepata hifadhi hapo, wakiwa ni familia, wagonjwa, watoto na wanawake. Maafisa wa Palestina wanasema zaidi ya watu 200 waliuliwa kutokana na shambulio hilo kubwa.


Kwa upande wake jeshi la Israel, IDF linakanusha kuhusika na shambulio hilo, likidai kwamba lilifanywa na kundi la wanamgabo la Islamic Jihad ambalo lilifyetua roketi ambayo haikufanikiwa kufyetuka kwenda mbali na kuangukia hospitali.


Kundi la Islamic Jihad limetoa taarifa likikanusha pia kuhusika na shambulio hilo.


Hapa Marekani, wizara ya ulinzi, Pentagon ilitoa taarifa ikisema kwamba haijapata bado uthibitisho juu ya nani alihusika na shambulio hilo lililotokea angani dhidi ya hospitali ya Al-Ahli Arab.


Hayo yakitokea White House ilitoa taarifa karibu na wakati ule ule ambao Rais Joe Biden anachukua ndege kuelekea Mashariki ya Kati, ikieleza kwamba Rais amesikitishwa na kukasirishwa sana baada ya kupata habari za shambulio hilo.


Taarifa inaeleza kwamba rais mara moja alituma rambi rambi zake kwa watu walouliwa ambao hawakua na makossa na kuwatakia walojeruhiwa afwen ya haraka.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad