Mshukiwa wa Mauaji ya Tupac Afikishwa Kortini

 

Mshukiwa wa Mauaji ya Tupac Afikishwa Kortini

 Mshukiwa wa Mauaji ya Tupac Afikishwa Kortini

Mshukiwa wa muuaji wa Tupac Shakur yaliyofanyika mwaka 1996 kwa kumpiga risasi amepandishwa kizimbani kwa mara ya kwanza katika Mahakama ya Nevada, Las Vegas nchini Marekani.


Duane "Keffe D" Davis, (60) alikuwa mshukiwa anayejulikana kwa muda mrefu katika kesi hiyo na alikiri hadharani kuhusika kwake katika mauaji hayo katika mahojiano kabla ya kumbukumbu yake ya 2019, "Compton Street Legend."


"Kuna jambo moja ambalo ni la uhakika unapoishi maisha ya kijambazi, tayari unajua kuwa vitu ulivyofanya vitakurudia, haujui ni kwa namna gani au lini, lakini hakuna shaka kuwa vitakurudia," aliwahi kuandika Davis 'Keffe D'.


Maoni hayo yalifufua uchunguzi wa polisi ambao ulisababisha kufunguliwa mashtaka ambapo mnamo Julai, polisi wa Las Vegas walivamia nyumba yake wakivuta hisia mpya kwenye mojawapo ya mafumbo ya kudumu ya muziki wa hip-hop.


Waendesha mashtaka wanadai kuuawa kwa Shakur kulitokana na ushindani wa utawala katika aina ya muziki ambayo wakati huo uliitwa "gangsta rap."


Aina hiyo ya muziki iliwakutanisha wanachama wa East Coast wa kundi la Bloods linalohusishwa na nguli wa muziki wa rap, Marion "Suge" Knight dhidi ya washiriki wa West Coast wa wanachama wa Crips ambalo Davis amesema aliliongoza huko Compton, California.


Kaka wa Tupac, Mopreme Shakur amesema familia hiyo ilikuwa na wasiwasi kama ipo siku haki ya ndugu yao itapatikana na kueleza kuwa mchakato huo usingecheleweshwa kama Tupac asingekuwa mweusi.


"Hatujasikia chochote kwa miaka 27. Binti yangu ana miaka 27 sasa, kwa hiyo uwajibikaji wowote katika hatua hii ni mzuri."

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad