Mwamba Mmoja Amuingizia Mkewe Panga Sehemu za Siri, Kisa Kahisi Kachepuka


Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamshikilia Mwanaume mmoja Mkazi wa Kijiji cha Makong'onda Wilaya ya Masasi Kwa tuhuma za kumjeruhi Mke wake Kwa kumpiga kisha kumuingizia panga sehemu ya haja kubwa.

“Tukio hilo limetokea October 08,2023, Mtuhumiwa pamoja na Mhanga baada ya kutoka kwenye mihangaiko yao ya kuokota korosho Mhanga alikwenda kwa Binamu yake kutwanga kisamvu ambapo ni eneo jirani na wanapoishi"

“Baada ya kukaa huko Kwa muda Mumewe alihisi ameenda kwa Mwanaume mwingine na ndipo baada ya kurejea alianza kumshambulia hadi Muhanga kupoteza fahamu, baada ya hapo Mtuhumiwa alichukuwa panga na kumuingizia Muhanga panga sehemu ya haja kubwa na kumsababishia majeraha"

“Mwanamke huyo anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Newala na hali yake inaendelea vizuri na Mtuhumiwa anatarajia kufika Mahakamani kujibu tuhuma zinazomkabili”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad