Mwanafunzi Ajiua Kwa Kujinyonga Akitaka Kuigiza Muvi

 

Mwanafunzi Ajiua Kwa Kujinyonga Akitaka Kuigiza Muvi

 Mwanafunzi Ajiua Kwa Kujinyonga Akitaka Kuigiza Muvi

Mwanafunzi wa darasa la sita shule ya msingi Majengo wilayani Same, mkoani Kilimanjaro Brian Elisha Godson (12) amejiua kwa kujinyonga akitaka kuigiza kama filamu ya kujinyonga aliyoipenda kuiangalia akiamini hatakufa.


Godson anadaiwa kufanya jaribio hilo kwa kujinyonga na shuka saa 12 asubuhi jana Jumamosi Septemba 30, mwaka huu, wakati bibi yake na ndugu zake wengine wakiwa wamelala.


Tukio hilo lilizua taharuki kubwa linatokea ikiwa zimepita siku 85 tangu rafiki yake na jirani yake Godson aitwaje Alex Mgonja mwanafunzi wa darasa la tano shule ya msingi ya Mtawa ya Mother Kelvin iliyopo Same kujinyonga kwa kutumia kitenge cha bibi yake aliyekuwa akiishi naye.


Bibi wa Godson, Endael Mhando, amesema mjukuuwake amekuwa akipenda kuangalia filamu za kutisha ‘Zombi’, akisema kuna siku moja alimweleza kuwa mtu anaweza kujinyonga na asife kutokana filamu hizo alizokuwa akiziangalia na wenzake.


“Alinambia kumbe unaweza kujaribu alafu ukatoka tuu vizuri, akanambia inawezakana yule mwenzetu aliyejinyonga ilikuwa ni bahati mbaya tuu maana kwenye filamu wanafanya hivyo lakini wanatoka na hawafi,”


Kaimu Kamanda wa polisi mkoa wa Kilimanjaro, Yahaya Mdogo amesema uchunguzi unaendelea kuhusu tukio hilo.


Akizungumzia tukio hilo, mkuu wa wilaya ya Same, Kasilda Mgeni amesema chanzo cha tukio hilo ni Godson amekuwa akipenda kuigiza filamu mbalimbali alizokuwa akipenda kuangalia kwenye runinga zinazohusu matukio ya kujinyonga.


Kasilda amesema matukio mengi yanayotokea wilayani humo kuhusu watoto imebainika kuwa wengi wao wanaishi na bibi zao, huku wazazi wengi hawako karibu na watoto wao, badala yake wapo mjini.


“Nitoe wito kwa wazazi kama ambavyo wamekuwa wakitafuta hawa watoto basi wajue wana haki ya kuwatunza na kuwalinda dhidi ya vitendo vinavowafanya watoe uhai wao.Hii imekuwa ni changamoto kubwa kwa watoto katika wilaya hii, wazazi wengi wameachia watoto bibi na babu zao


“Tutaandaa mpango wa kuangalia wa namna Serikali tunawasaka wazazi hawa ili kuwajibika kwa watoto wao, kwa sababu baadhi yao wanakaa bila wazazi wakati ni haki yao kulindwa,”amesema.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad