Mwanamuziki Jux Akiri Kuumia Vanessa Mdee Alipobeba Mimba ya Rotimi

Mwanamuziki Jux Akiri Kuumia Vanessa Mdee Alipobeba Mimba ya Rotimi

Mwanamuziki Jux Akiri Kuumia Vanessa Mdee Alipobeba Mimba ya Rotimi

Mwimbaji maarufu wa Bongo R’n’B Juma Jux amekiri kuwa alihuzunika sana alipopata taarifa kwamba mpenzi wake wa zamani Vanessa Mdee alikuwa akitarajia mtoto wake wa kwanza na mpenzi wake wa sasa, Olurotimi Akinosho almaarufu Rotimi mnamo Septemba 2021.


Jux alikuwa akiimba wimbo wake wa ‘Sina Neno’ alioutoa zaidi ya miaka miwili iliyopita baada ya Vanessa kuzaa mtoto wake wa kwanza alipofunguka kuhusu jinsi jambo hilo lilimfanya ajisikie.


Baada ya kuimba maneno kadhaa ya wimbo huo, mashabiki waliokuwa wamejitokeza kumtazama akitumbuiza walimuuliza iwapo Vanessa kupata mtoto na mwanaume mwingine ilimuumiza na bila aibu akakiri kuwa aliumia sana.


"Niliumia. Sio mchezo niliumia kweli. Watoto wa hii town wana balaa kweli. Wakati huo niliumia sio mchezo,” Jux alisema.


Vanessa Mdee, ambaye alichumbiana na Jux kwa takriban miaka sita kabla ya kutengana naye mwaka 2019, alipata mtoto wake wa kwanza na muigizaji na mwimbaji wa Kimarekani mwenye asili ya Nigeria, Rotimi mwezi Septemba 2021 baada ya wawili hao kuwa na mahusiano ya kimapenzi kwa takriban mwaka mmoja.


Muda mfupi baada ya Vanessa Mdee kutangaza kuwa ni mjamzito zaidi ya miaka miwili iliyopita, Jux alitoa wimbo wa kumpongeza.


Kwenye wimbo huo 'Sina Neno', Jux alimhakikishia Mdee kuwa hana ugomvi wowote naye kwani alishafunika yaliyopita kwenye kaburi la sahau.Alisema kuwa ana raha sana kuona kuwa Mdee anafurahia ndoa yake ya sasa na muigizaji Rotimi na kumpongeza kwa kuwa alikuwa karibu kuitwa mama.


Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad