Mwimbaji Omah Lay Atoa Mpya, Adai Aamini Tena Katika Mungu Baada ya Kupata Mkwanja



Baada ya kuanza kutengeneza pesa, siamini tena katika dini wala kufurahia dini, namuamini zaidi Mungu, kumheshimu Mungu na nimekuwa binadamu zaidi kuliko kuwa mtu wa dini - Omah Lay

Katika mahojiano yake mapya mwanamuziki huyo maarufu wa Nigeria, alipoulizwa na mtangazaji, amesema kwamba yeye alikulia katika familia ya kikiristo na muda mwingi alikuwa anaenda kanisani, na kuna kipindi alifikiria kubadili dini kutaka kuwa muislamu, lakini pia ikafikia muda akaona ni bora zaidi yeye awe karibu na Mungu na sio kuwa karibu na dini zilizopo

Anasema anajua vitabu vya dini vipo, vyote vinavyosemwa na kila mtu anachosema kuhusu dini inaonekana kweli ila hana uhakika kwasababu ushahidi hauoni, hana uhakika kama kweli hivyo vitabu viliandikwa na Mungu au watumishi wa Mungu mwenyewe

Hivyo, ameona aache kuweka mkazo katika mitazamo/mambo ya dini ila ajikite zaidi kumuamini Mungu na kumheshimu Mungu kuliko kuamini dini, na yeye kwasasa amekuwa more human than religious

Amesema yeye ushahidi wake kuwa Mungu yupo ni sababu anamsaidia kujongea, hajui kwa namna gani mwili wake unajongea na hicho ndicho kinachofanya aamini kuna mtu anawezesha hilo na huyo ndie Mungu ambaye ameamua kumuamini na kumheshimu

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad