Naira Marley, Sam Larry kortini kwa mauaji ya Mohbad, wasweka rumande

Naira Marley, Sam Larry kortini kwa mauaji ya Mohbad, wasweka rumande


Video iliyopostiwa mtandaoni na mwigizaji wa Nollywood, Tonto Dikeh imemuonyesha bosi wa Lebo ya Marlian, Azeez Fashola, maarufu kama Naira Marley na msaidizi wake, Balogun Eletu, anayejulikana pia kama Sam Larry wakitoka mahakamani baada ya kurudishwa rumande.


Ikumbukwe kwamba wawili hao waliwekwa chini ya ulinzi wa polisi na Mahakama ya Hakimu iliyoketi katika eneo la Yaba katika Jimbo la Lagos siku ya Jumatano kwa tuhuma za kuhusika na kifo cha aliyekuwa staa wa muziki nchini humo, Ilerioluwa Oladimeji Aloba, maarufu kama MohBad.


Taarifa kutoka nchini humo zinaeleza kuwa, Jeshi Polisi katika Jimbo la Lagos limeomba Naira Marley na wenzake wengine wazuiliwe kwa siku 30 wakisubiri kukamilika kwa uchunguzi wa kesi yao.


Hakimu Adeola Olatunbosun, hata hivyo, aliamua kwamba Fashola na wenzake wazuiliwe kwa siku 21 pekee.


Akijibu tukio hilo, Tonto aliposti video ya Naira Marley na Sam Larry wakitoka mahakamani na nukuu inasema, "Naira Marley na Sam Larry wamerudishwa rumande kwa siku 21.


"Kwa wakati huu ningependa kusema asante kwa hakimu."


Kumbuka kwamba Naira Marley Jumanne alitangaza kurejea Nigeria kusaidia uchunguzi wa kifo cha Mohbad.


Mwimbaji huyo mwenye utata alifichua habari kuhusu kurejea kwake katika chapisho siku ya Jumanne kupitia akaunti yake kwenye jukwaa la X (zamani lilijulikana kama Twitter).


Aliandika, "Ningependa kushiriki kwamba nimefika tu Lagos, Nigeria kusaidia mamlaka na uchunguzi unaoendelea. Ni muhimu nifanye sehemu yangu kwa Imole. Nitakutana na polisi nikiwa na matumaini ya ukweli kufichuliwa na haki itatendeka.”

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad