Papa: Kanisa Katoliki Kubariki Wapenzi wa Jinsia Moja




"Hatuwezi kuwahukumu ambao wanakanusha tu, kukataa na kuwatenga,"
-
Kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani Papa Francis amependekeza kuwa atakuwa tayari kuona Kanisa Katoliki likibariki wapenzi wa jinsia moja.

Akijibu kundi la makadinali waliomuomba ufafanuzi juu ya suala hilo, alisema ombi lolote la baraka linapaswa kushughulikiwa na "hisani ya kichungaji".

Aliongeza, hata hivyo, Kanisa Katoliki bado linachukulia uhusiano wa jinsia moja "kuwa dhambi" na halitatambua ndoa za jinsia moja.

Ombi hilo lilikuwa mojawapo ya maombi yaliyotumwa kwa Papa kabla ya mkutano wa kimataifa wa wiki nzima kujadili mustakabali wa Kanisa unaotarajiwa kuanza mjini Vatican siku ya Jumatano.

Katika Kanisa Katoliki, baraka ni maombi au ombi, ambalo kwa kawaida hutolewa na kiongozi wa kiroho, akimwomba Mungu amtazame mtu au watu wanaobarikiwa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad