Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), imetangaza bei kikomo za bidhaa za Mafuta zilizoanza kutumika leo Oktoba 4, 2023 ambapo kwa Dar es Salaam Petroli ni Tsh. 3,281, Dizeli 3,448 na Mafuta ya Taa Tsh. 2,943 ikiwa na ongezeko la Tsh. 68 kwa kila Lita ya Petroli
Tanga, Petroli ni Tsh. 3,327, Dizeli 3,494, Mafuta ya Taa Tsh. 2,989 na Mtwara, Petroli itauzwa Tsh. 3,353, Dizeli Tsh. 3,520 na Mafuta ya Taa Tsh. 3,016 ambapo EWURA imesema ongezeko hilo linatokana na kupanda kwa 4.21% ya Gharama za Mafuta katika Soko la Dunia
Aidha, EWURA imesema gharama za uagizaji Mafuta zimepanda hadi kufikia 17% kwa Petroli, 62% kwa Dizeli na 4% kwa Mafuta ya Taa. Pia, Bei za Mafuta zimeathiriwa na uamuzi wa wazalishaji wakubwa wa Mafuta duniani (OPEC+) waliopunguza uzalishaji pamoja na vikwazo vya kiuchumi vilivyowekwa dhidi ya
Urusi