Prime Boy Asakwa Kifo cha MohBad

 

Prime Boy Asakwa Kifo cha MohBad

 Prime Boy Asakwa Kifo cha MohBad

Jeshi la Polisi Jimbo la Lagos limetangaza kuwa Owodunni Ibrahim a.k.a. Prime Boy anatafutwa kufuatia kushindwa kuheshimu mwaliko wa polisi kwaajili ya upelelezi na kushindwa kutokea kusaidia jeshi la polisi katika uchunguzi wa kifo cha Mohbad.


Taarifa iliyotiwa saini na Kamanda wa Polisi wa Lagos Benjamin Hundeyin ilisomeka kuwa "Ibrahim ana urefu wa takriban mita 1.64 mwanamume mwenye rangi nyeusi na alama za kikabila na kabila la Yoruba.


Anwani yake ya mwisho inayojulikana ni 3rd Power Oke Eletu Ikorodu.Akionekana wasiliana na kituo cha polisi kilicho karibu nawe au piga 0803 688 5727.


Pia jeshi la Polisi Nigeria limeahidi kutoa ofa ya N1M ( Tsh Milioni 3.2/=) kwa atakayetoa taarifa kamili itakayosaidia jeshi la polisi kufanikisha kukamatwa kwake.


Taarifa zinasema Prime Boy anatafutwa kutokana na taarifa kuwa alimjeruhi Mohbad kwenye Party huko Ikorodu na ndo siku hiyo hiyo alifariki dunia.


Pia, Mwimbaji mkongwe wa Nigeria, John Odafe Asiemo almaarufu Daddy Showkey amefichua kuwa amekuwa akipokea vitisho vya kuuawa kufuatia maoni yake kuhusu kifo cha rapa Mohbad baada ya kusema baadhi ya watu wenye nguvu katika tasnia ya muziki wanahusika kwenye kifo cha Mohbad.


Comments:

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad