Licha ya vita vikiendelea baina ya Israel, na wanamgambo wa Hamas, katika ukanda wa Gaza, rais wa Marekani, Joe Biden, Jumatano ametoa kauli ya kuunga mkono kile kilichoonekana kama lengo la mbali la suluhisho la kuunda mataifa mawili ya Israel na Paletina.
Rais Biden, akiwa katika mkutano na wanahabari White House, amesema kwamba matamanio ya Wapalestina hayapaswi kupuuzwa.
Israel, na Palestina, ameomgeza kusema kwamba zinastahili kuishi kama majirani kwa usalama, utu na amani.
Kiongozi huyo wa Marekani amesema ameshtushwa na walowezi wenye msimamo mkali wanao washambulia Wapalestina katika makazi ya Walowezi ndani ya ukingo wa magharibi.
Amesema vitendo hivyo ni kuendelea kuchochea moto, na kwamba Walowezi wanawashambulia Wapelestina katika maeneo wanayostahili kuwepo.
Pia aligusia wasiwasi wake kuhusiana na mateka 200 walio chini ya Hamas, baadhi yao wanaaminika kuwa Wamerekani.