Rais wa Marekani, Joe Biden Achukizwa na Mauaji Hospitalini


Rais wa Marekani, Joe Biden amedai amechukizwa na mashambulizi dhidi ya Hospitali moja katika Ukanda wa Gaza, ambayo yameuwa zaidi ya Watu 500 na kusababisha ukosoaji mkali kutoka Mataifa na Mashirika mbalimbali.

Mtandao wa @DW_Kiswahili umeripoti kuwa Biden ameyasema hayo mara tu baada ya kuwasili nchini Israel na kukutana na Mwenyeji wake, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu, leo Jumatano October 18,2023.

Rais huyo wa Marekani amelituhumu kundi la Wanamgambo wa Kipalestina la Hamas kuwa limehusika kufanya shambulizi hilo la Hospitali

Biden amesema Nchi yake itaipa Israel kila kitu inachohitaji kujilinda yenyewe wakati ikiendeleza vita vyake dhidi ya Hamas.

Israel inadai shambulizi hilo limesababishwa na roketi ya Palestina lakini Hamas inakanusha madai hayo.

Biden amedai kundi la Hamas ni baya zaidi kuliko kundi linalojiita Dola la Kiislamu kwa kitendo chao cha kuwaua Raia wa Israel katika shambulizi la October 07.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad