Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila, ametoa kauli hiyo wakati akiwasilisha Taarifa ya Kamati iliyoundwa kwaajili ya kuchunguza chanzo cha Moto uliotokea Oktoba Mosi, 2023 Kariakoo jijini Dar es Salaam
Chalamila amesema Kamati imebaini Moto huo haukutokana na ajali, bali ni hujuma za Wafanyabiashara wenyewe ambapo Moto ulianzia katika eneo la Mnadani (Kariakoo Auction Mart) na haukusababishwa na Jenereta kama ilivyodaiwa awali
Ameongeza "Kamera za CCTV zilizokuwa pembeni ya majengo wakati Moto unaanza zimeonesha Jenereta linalodaiwa kuwa chanzo cha Moto ni zima, linafanya kazi na halikuungua"