Robertinho Afunguka Sababu ya Kumtumia Bocco Kuiuwa Dynamos

 

Robertinho Afunguka Sababu ya Kumtumia Bocco Kuiuwa Dynamos

Kocha Mkuu wa Simba Roberto Oliveira 'Robertinho' amesema kwa kiasi kikubwa benchi la ufundi pamoja na wachezaji wamefurahi kuingia hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.


Robertinho amesema hayop jana mara baada ya kumalizika kwa mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika na kufanikiwa kutinga hatua ya makundi ya michuano hiyo kwa kutoa sare ya bao 3-3 na Power Dynamos ya Zambia.


Mbrazil huyo amesema mchezo wa kufuzu hatua ya makundi si rahisi na wamekutana na mpinzani ambaye kwenye dakika zote wametoka sare.


“Champions League hakuna mechi nyepesi, mechi zote ni ngumu. Nimejiandaa wiki yote hii kwa mbinu mpya kwenye kipindi cha pili. Kama wachezaji wangu wanapokuwa wamechoka ninaamua kumtumia Bocco.


“Nimecheza na washambuliaji wawili, Kibu na baleke lakini ninahitaji straika mmoja kweye boksi, Bocco ameweza na tumepata matokeo kwa hiyo kama mwalimu naweza kudiriki kusema mabadiliko yangu yamenisaidia.


“Tulifunga viungo wa mpinzani wangu, walikuwa zero. Nilichokifanya ni kufunga viungo na kumuweka Bocco kwenye boksi. Nimepoteza nafasi zaidi ya tano ndani ya boksi.


“Nyakati zote ninapocheza Champions League nikiwa Uganda, Rwanda nimekuwa nikifanikiwa kutinga makundi. CAFCL sio sawa na mechi za Ligi. Hii ni heshima kubwa kwa Simba. Ninafuraha sana kwa sababu haikuwa rahisi.


“Leo kosa moja, wapinzani wetu walikuwa zero, nilichokifanya ni kusahihisha makossa, nikampa nafasi Bocco. Baada ya hapo tumekwenda makundi.


“Kila mmoja sasa hivi analizungumzia soka la Tanzania. Nina wachezaji wenye uzoefu na wachezaji vijana, lazima uwape nafasi wote kwa ajili ya manufaa ya Simba ijayo.


“Malengo yangu ni kucheza soka safi. Kama nina vijana wenye vipaji nitawatumia, nitawatumia Chama, Onana, Saido kwa sababu wana vipaji na ni hatari kwa adui wangu," amesema Robertinho.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad