Kocha mkuu wa Simba SC Robert Oliveira “Robertinho’ amefunguka kurejea kwa mastaa wake waliokuwa kwenye majukumu ya timu za Taifa kumewaongeza nguvu ya maandalizi.
Simba watavaana na Al Ahly leo ljumaa (Oktoba 20) katika mchezo wa ufunguzi wa mashindano ya African Football League unaotarajiwa kufanyika kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es salaam.
Baadhi ya mastaa wa Simba SC ambao walikuwa na majukumu ya timu za Taifa ni pamoja na Mzamiru Yassin, Ally Salim, Israel Mwenda, Henock Inonga, Clatous Chama na Kibu Denis.
Robertinho anaingia katika mchezo huu akiwa ameiongoza Simba SC kuandika rekodi ya kuwa timu pekee ya Ligi Kuu Bara msimu huu ambayo imefanikiwa kuandikisha ushindi wa asilimia 100 baada ya kushinda michezo yao yote mitano ya kwanza.
Robertinho amesema: “Ni jambo zuri kuona baadhi ya mastaa wetu ambao walikuwa na majukumu ya timu za Taifa wamerejea kuripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo huu, tunajua utakuwa mchezo mgumu lakini ari yetu imeongezeka.”