Rose Ndauka Amechagua Maisha yake, Ustaa Kaweka Pembeni..

 

Rose Ndauka Amechagua Maisha yake, Ustaa Kaweka Pembeni..

Inawezekana pengine ulikuwa unajiuliza Rose Ndauka yuko wapi? mbona haonekani kwenye sherehe za mastaa wenzake? mbona hasikiki? mbona havumi? Mbona hachafui hali ya hewa?


Mbona haonekani kwenye Filamu mpya na Tamthilia zinazofanya vizuri? Yuko wapi Ndauka mwanamke mrembo aliyetikisa kwa uhodari wake wa kuigiza, macho mazuri na figa za kuvutia.


Basi majibu ya hayo maswali yako ni kwamba Rose Ndauka yupo na anaendelea na shughuli zake kama kawaida ingawa siyo shughuli za kisanaa.


Ameolewa na mpaka sasa ana watoto watatu ambapo mtoto wake wa tatu ametimiza siku 40 hivi karibuni tangu alipozaliwa na kati ya hao watoto wa kike ni mmoja wawili ni wa kiume.


Ndauka na mume wake Haffiyy wana kampuni yao inayoitwa (HRD RADIATOR COMPANY) ambapo huko ndiyo wanajichumia pesa zao. Lakini pia ana miradi yake mingine ya siri ambayo hajaamua kuiweka wazi.


Ndauka amechagua kuwa mama wa kawaida hajaupa Ustaa kipaumbele, ndoa imembadilisha kwa kiasi kikubwa na hii ni kwasababu pia amepata mume mwenye nia na malengo na wanapendana wenyewe.


Ndauka wa sasa si yule Ndauka machachali wa enzi za magazeti wa nusu uchi na skendo mfululizo. Amejitenga na ulimwengu wa mastaa wenzake wa kike, yupo kwenye maisha ya kawaida lakini yenye wadhifa.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad