Sababu za Tanasha Kupendekezwa Kuolewa na Diamond Platnumz

Sababu za Tanasha Kupendekezwa Kuolewa na Diamond Platnumz


Mwanamitindo wa Kenya, Tanasha Donna anapendekezwa na kutajwa na wengi kuwa anafaa kuolewa na Diamond Platnumz, ambaye tayari wamejaliwa mtoto mmoja, Naseeb Junior kabla ya kuvunjika kwa uhusiano wao.


Hiyo ni baada ya hapo juzi Diamond kusherekea siku yake ya kuzaliwa (birthday) na Naseeb Junior ambaye wamezaliwa siku moja, Oktoba 2 ila miaka tofauti.


Utakumbuka Tanasha na Diamond walikuwa na uhusiano kati ya mwaka 2018 hadi 2020 walipoachana huku wakiwa na mtoto huyo mmoja, Naseeb Junior aliyezaliwa Oktoba 2019.


Kabla ya Tanasha, tayari Diamond aliwahi kuwa na uhusiano wanawake wengine maarufu Afrika Mashiriki, miongoni mwao ni Zari The Bosslady (Uganda) aliyejaliwa naye watoto wawili na Hamisa Mobetto (Tanzania) mwenye mtoto mmoja naye.


Picha alizochapisha Staa huyo wa WCB Wasafi katika mitandao yake ya kijamii jana akiwa na mtoto wake zimeibua maoni ya wengi ambao wanasema jinsi ambavyo wanafanana, basi Tanasha anafaa kuwa mke wake halali wa ndoa.


"Kusherekea siku yangu ya kuzaliwa na mtoto wangu wa mwisho ni jambo zuri na la baraka zaidi ambalo zimewahi kulifikiria." aliandika Diamond ambaye ni Baba watoto watano hadi sasa.


Sababu nyingine kwanini Tanasha anapigiwa chupuo, ni kutokana naye amezaliwa siku moja na mama mzazi wa Diamond, Mama Dangote, tarehe zao za kuzaliwa ni Julai 7, Tanasha akiwa amezaliwa mwaka 1995, huku Mama Dangote ikiwa ni 1971.


Na hadi sasa hakuna mwanamke ambaye amewahi kufanyiwa 'birthday party' kubwa na Diamond kama Tanasha, birthday yake ya mwaka 2019 pale Mlimani City, Dar es Salaam, Diamond alimzawadia Tanasha gari jipya aina ya Toyota Land Cruiser V8.


Ikumbukwe Tanasha baba yake ni raia wa Italia na mama akitokea Kenya, akiwa na miaka 11 alihamia Ubelgiji kusoma na baadaye alivutiwa na mitindo, alirejea Kenya ili kushiriki mashindano ya urembo kabla ya utangazaji na muziki.


Sababu ya tatu kwanini Tanasha anapendekezwa, ni kwamba tangu kuachana kwake na Diamond zaidi ya miaka miwili iliyopita, hajawahi kuweka rasmi wazi mahusiano yake mapya kwa umma.


Hiyo ni tofauti na wanawake wengine waliozaa na Diamond, Zari The Bosslady tayari ameolewa na Shakib Chams kutokea Uganda, huku Hamisa Mobetto akiwa na uhusiano na Kevin Sowax kutoka nchini Togo.


Na Diamond tangu kuachana na Tanasha hajaweka wazi mahusiano yake licha ya kuwepo madai kuwa yupo na Zuchu ila ukitazama historia ya Diamond tangu yupo na Penny, Wema Sepetu, Zari hadi Tanasha, kwa Zuchu utaona utofauti mkubwa wa mambo jinsi yanavyoenda.


Ikumbukwe Tanasha ambaye pia anafanya muziki ameshikiriana na Diamond katika wimbo, Gere kutoka katika EP yake ya kwanza, DonnaTella (2020) iliyoshirikisha wasanii wengine kama Mbosso (La Vie) na Khaligraph Jones (Ride) kutokea Kenya.

Post a Comment

0 Comments
* Please Don't Spam Here. All the Comments are Reviewed by Admin.

Top Post Ad

Below Post Ad